Tuesday, 30 October 2018

 ubunifu na kujituma ndo kila kitu mtaji utaongezeka tu

Ubunifu na kujituma ndio kila kitu
Mtaji utaongezeka tu..
Na,Seth

                         
Nikweli mtaji ni kitu muhimu kwenye kila biashara lakini kuna mambo mengine ya kuzingatia ili biashara yako iweze kusimama vizuri unapaswa kuwa 1.mbunifu
         2.Juhudi
Ubunifu ndo kila kitu kwenye biashara,ili uweze kushindana na biashara nyingine ambazo zipo sawa na yakwako unapaswa kuwa mbunifu ili uweze kuvutia wateja Zaidi kuwa mbunifu kuta kupa faida nyingi kama,
                                      
   1.Kuwa na bidhaa zenye sifa za ziada kuliko bidhaa za washindani wako,hii itakufanya kuongeza wateja wako na kupanua mipaka ya soko lako hivyo  kuwa na namba kubwa ya mauzo kwa siku na kukufanya  kupata faida kubwa na kuongeza mtaji wako.
2.kutengeneza bidhaa zinazo waridhisha wateja wako,hii itakufanya uwe juu kwani hakuna mtu anae penda kitu kisicho kata kiu yake hivyo ni Dhahiri watu watatumia bidhaa zako Zaidi.
3.utaweza kutofautisha biashara yako na zingine ,kama biashara yako ina vitu vya kipekee vinavyo tokana na ubunifu ni wazi itakua bora Zaidi ya nyingine hivyo itakuwia rahisi hata kwenye kuitangaza kwana ina sifa za ziada.
Kujituma ni jambo la muhimu Zaidi kwani kufanya kazi kwa bidi daima inalipa(jasho la mtu halipotei bure)
                          
Ukiwa unajituma ni wazi utafanikiwa licha ya mtaji wako kuwa mdogo kwani watuwengi walio fanikiwa wamefanya kazi kwa bidi hadi kufika hapo walipo hawakuanzia juu walipanda juu,unahitaji uvumilivu tu changamoto zipo lakini unaweza kabiliana nazo na ukafika mbali Zaidi kuliko wale wanaofanya mambo kawaida tu.
Ukifanya hayo mambo mawili mtaji hautokua kikwazo bali changamoto ya kawaida tu kwani wapo walio anza na elfu 15 leo wako mbali kibiashara hivyo kazi ni kwako kuanza sasa.