Ubunifu na
kujituma ndio kila kitu
Mtaji
utaongezeka tu..
Na,Seth

Nikweli
mtaji ni kitu muhimu kwenye kila biashara lakini kuna mambo mengine ya
kuzingatia ili biashara yako iweze kusimama vizuri unapaswa kuwa 1.mbunifu
2.Juhudi
Ubunifu ndo
kila kitu kwenye biashara,ili uweze kushindana na biashara nyingine ambazo zipo
sawa na yakwako unapaswa kuwa mbunifu ili uweze kuvutia wateja Zaidi kuwa
mbunifu kuta kupa faida nyingi kama,

1.Kuwa na bidhaa zenye sifa za ziada kuliko
bidhaa za washindani wako,hii itakufanya kuongeza wateja wako na kupanua mipaka
ya soko lako hivyo kuwa na namba kubwa
ya mauzo kwa siku na kukufanya kupata
faida kubwa na kuongeza mtaji wako.
2.kutengeneza
bidhaa zinazo waridhisha wateja wako,hii itakufanya uwe juu kwani hakuna mtu
anae penda kitu kisicho kata kiu yake hivyo ni Dhahiri watu watatumia bidhaa
zako Zaidi.
3.utaweza
kutofautisha biashara yako na zingine ,kama biashara yako ina vitu vya kipekee
vinavyo tokana na ubunifu ni wazi itakua bora Zaidi ya nyingine hivyo itakuwia
rahisi hata kwenye kuitangaza kwana ina sifa za ziada.
Kujituma ni
jambo la muhimu Zaidi kwani kufanya kazi kwa bidi daima inalipa(jasho la mtu
halipotei bure)
Ukiwa
unajituma ni wazi utafanikiwa licha ya mtaji wako kuwa mdogo kwani watuwengi
walio fanikiwa wamefanya kazi kwa bidi hadi kufika hapo walipo hawakuanzia juu
walipanda juu,unahitaji uvumilivu tu changamoto zipo lakini unaweza kabiliana
nazo na ukafika mbali Zaidi kuliko wale wanaofanya mambo kawaida tu.
Ukifanya
hayo mambo mawili mtaji hautokua kikwazo bali changamoto ya kawaida tu kwani
wapo walio anza na elfu 15 leo wako mbali kibiashara hivyo kazi ni kwako kuanza
sasa.
0 coment�rios: