Mambo muhimu Kwa kila kijana mwenye Ndoto ya kua mjasiriamali bora.
Kwanza kila kijana mwenye ndoto ya kua mjasiriamali bora anapaswa kufahamu kwamba umri aliopo ndio umri sahihi wakuanza kutimiza ndoto zake kwasababu…(1)Bado majukumu hayajawa mengi
(2)Ana mda mrefu bado wakujaribu shughuli
Mbalimbali….(sio kila jambo utakalo lifanya litafanikiwa)
(3)Ana nguvu za kutosha kufanya kazi yoyote
na uwezo mkubwa wa kufikiria .
Mambo ya kuzingatia ili ufanikiwe.
.Chagua biashara sahihi kulingana na mazingira na wakati,unaweza kua una kila sifa ya kua mjasiriamali bora lakini kushindwa kuchagua biashara sahihi ya kufanya kulingana na mazingira na wakati kuka fanya usifanikiwe hivyo kabla ya kuchagua biashara ya kufanya unapaswa ujue(wateja wako,kipato cha wateja wako,Imani na mila na desturi za wateja wako na wastani wa umri wa wateja wako)hio itakusaidia kuchagua biashara inayo endana na wateja wako.
. Penda kitu unacho kifanya,kama unapenda kitu unacho kifanya ni wazi utakifanya kwa moyo na kwa bidii hivyo utafanikiwa kwani penye nia pana njia.
.Nidhamu ya fedha na kazi,licha ya kuipenda kazi(biashara) unayo ifanya unapaswa kuiheshimu pia na kuzingatia vitu kama(mda wa kazi,mahusiano na wateja,muonekano kulingana na kazi yako…)pia unapaswa kuheshimu fedha unazo zipata na kufanyia mambo ya muhimu kuliko kuzitumia kwenye starehe na vitu visivyo na ulazima kwa wakati huo kwani unaweza kua unafanya kitu sahihi kwa wakati ambao si sahihi,hivyo itakua ngumu kwako kufanikiwa.
.Jifunze kuweka akiba,ni vizuri kwenye kila kidogo unacho kipata uweke akiba kwani sio kila wakati biashara yako itakua hivyohivyo kuna kupanda na kushuka kwenye biashara hivyo akiba yako itakusaidia wakati mambo hayapo sawa na pia itakusaidia kuongeza mtaji.
.Wajue washindani wako (udhaifu na ubora wao) hio itakusaidia kujua mambo ya kufanya ili uweze kuwaridhisha wateja wako na kuwavutia wateja Zaidi hivyo itakusaidia kuwa na wateja wengi Zaidi.
Changamoto ambazo huna budi kuzikabili
Ili utimize malengo yako.
Lazima utambue kwamba mambo hayatokua rahisi tena kwa kijana ambae ndo kwanza una anza kujihusisha na ujasiriamali hivyo huna budi kukabiliana na changamoto kama….
.mtaji mdogo,kutokana na ni mara ya kwanza unajihusisha na biashara kuna gharama ambazo hukuzitegemea zita jitokeza hivyo kufanya hesabu zako kutokwenda sawa
.Namba ya wateja kuwa ndogo kulinganisha na matarajio yako,hii inaweza kutokea haswa pale biashara inapokua mpya kwani itakubidi kuvumilia na kufanya njia mbalimbali kama(kutangaza biashara yako,kuwa na ofa au kuuza bei ya chini kulinganisha na washindani wako).hio itakusaidia kuongeza namba ya wateja.
.Faida kuwa ndogo au kutoipata kabisa,pindi unapokua una anza biashara flani unaweza kuifanya kwa kipindi flani bila kupata faida ambayo ulitegemea au kuhadisiwa kua watu wanao fanya hio biashara wanaipata hivyo unapaswa kuwa mvumilivu na mambo yataenda sawa.
.Aina ya wateja nayo huwa ina wakwaza watu wengi ambao ndio wana anza biashara,unaweza kuwa na wateja wakorofi sana na wenye lugha chafu na za kukera hivyo unapaswa kuwa mvumilivu na kujua jinsi ya kukabiliana nao.
Jinsi ya kukabiliana na hizo changamoto…
.Uvumilivu ni moja kati ya vitu vitakavyo kusaidia kudumu katika biashara unayo ifanya na kupambana na kila changamoto.
.Ubunifu,utakufanya uwe bora na uwazidi washindani wako kwa kuwavutia wateja wengi Zaidi.
.Mwonekano,utakusaidia kuwa na mvuto kwa wateja kwani wateja wengi wana vutiwa na mtu mwenye mwonekano safi na nadhifu.
.Aina ya lugha unayo tumia,unapaswa kutumia lugha nzuri na ya unyenyekevu itakayo wavutia wateja wako na kuwafurahisha
Kila mtu anapenda kufanikiwa ila tatizo lipo kwenye kufanya mambo yatakayo mfanya afanikiwe,na matumizi mazuri ya fursa, na kufata ushauri ulio bora.Hivyo kama kijana unapaswa kuyazingatia haya kabla huja anza ujasiriamali kwani yatakufikisha mbali.
Name:WALTER SETH

0 coment�rios: